Add parallel Print Page Options

30 Alipoionja ile siki, akasema, “Imekwisha.” Baada ya hapo akainamisha kichwa chake na kufa.

31 Hii ilikuwa Ijumaa, Siku ya Matayarisho. Siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya Sabato maalumu. Viongozi wa Kiyahudi hawakuitaka ile miili ya waliosulubiwa ikae juu misalabani katika siku ya Sabato. Hivyo wakamwomba Pilato atoe amri kuwa miguu ya wale watu misalabani ivunjwe. Pia wakaomba ile miili ishushwe kutoka kwenye misalaba. 32 Kwa hiyo askari wakaja na kuivunja miguu[a] ya watu wale wawili kwenye misalaba kando ya Yesu.

Read full chapter

Footnotes

  1. 19:32 kuivunja miguu Miguu ilivunjwa ili kuwafanya wale waliokuwa misalabani wafe haraka zaidi.